Home Education Sifa za Wahusika Katika Riwaya Kigogo na Pauline Kea

Sifa za Wahusika Katika Riwaya Kigogo na Pauline Kea

7

Pata maelezo kamili ya Sifa za Wahusika Katika Riwaya Kigogo na Pauline Kea.

  • Kigogo Riwaya
  • Maswali YaKigogo
  • MwongozoWa Kigogo
  • Sifa Za Ashua KatikaKigogo
  • Sifa Za Majoka
  • Sifa Za Tunu KatikaKigogo
  • Tamthilia YaKigogo
  • UchambuziWa Kigogo

Sifa Za Tunu KatikaKigogo

Baadhi ya Sifa za Tunu:
1. Msomi- Ana shahada ya. udaktari katika sheria inayomwezesha kutetea haki za wanasagamoyo.
Mwenye Msimamo thabiti – Licha ya kuvamiwa na kuvunjwa mguu na Uongozi wa Majoka halegezi Msimamo wake wa kutetea Wanasagamoyo.
Jasiri – Licha ya kutishiwa na Majoka kuwa angemwangamiza hasitishi upinzani wake.
– anamfuata Majoka Hadi kwake kumwambia awafungulie soko la Chapakazi.
Mtetezi- Anaanda maandamano ya kushinikiza kufunguliwa kwa soko la Chapakazi kwa ushirikiano na Sudi.

UMUHIMU WAKE UTOKANE NA SIFA ZAKE:
1. Anaendeleza maudhui ya elimu kwa kusomea udaktari wa sheria.
2. anaendeleza maudhui ya nafasi ya mwanamke kama vile jasiri, mkombozi, msomi- no.
1. Anajenga sifa za Majoka mfano katili- anapowatuma majambazi kumvamia na kumvunja mguu.

JALADA – Kigogo
Jalada ni picha iyoko mbele ya tamthilia hi ya “Kigogo”
Kuna picha ya mtu wa kiume aliyeketi kwenye kiti akiwa ameshikilia kidevu chake na Rungu mknoni.
– Kiti Ni ishara ya Uongozi. kwa hivyo kiti alichokalia Ni ishara kuwa yeye ndiye amekalia kiti Cha Uongozi hususani wa Sagamoyo.
– Rungu aliyoshikilia mkononi ni ishara ya mamlaka aliyo nayo. 
– Amefunikwa na rangi nyeusi kuashiria kuwa Ni kiongozi wa kiafrika.
– Ameshika kidevu Kama ishara kuwa anawazia Jambo Fulani hususani upinzani wake Tunu unaotatiza Uongozi wake.
Kuna ramani ya Afrika walimosimama watu wanaotazamwa na mtu huyu.
– Hii ni ishara kuwa hawa Ni watu kutoka mataifa ya Kiafrika waluoathirika na Uongozi mbaya wa Baada ya kuondolewa kwa mzungu.
-wamefunikwa na wingu jeusi kuashiria matatizo yanayowakumba watu weusi yakisababishwa na Uongozi kutoka kwa viongozi wao wa kiafrika mfano soko la Chapakazi walilolitegemea kwa kila namna linafungwa na Majoka.
Nyuma na umati huo wa watu Kuna mwangaza mkubwa unaowamlika Kama ishara ya matumaini yanayoletwa na Tunu kujitolea kupigania haki za Wanasagamoyo Hadi kumwondoa Majoka uongozini.

Uchambuzi wa jalada la KIGOGO.
Kitabu hiki ni Tamthilia ambacho ni mara ya kwanza kuidhinishwa katika shuke za upili hapa nchini Kenya.

Kimeandikwa na Pauline Kea…

Michoro ipo kwenye jalada lake na ni kama ifuatavyo:
+Mchoro wa ramani ya Afrika uliochorwa kwa rangi nyeusi. Mchoro huu ni ishara wazi kuwa manthari husika ni Afrika.

+Mchoro wa watu waonekanao kama vivuli kwenye mchoro wa ramani ya Afrika. Pia ni rangi nyeusi kiashiria cha watu wa bara la Afrika.

+Mchoro wa jua lichomozalo hasa nyuma ya ule mchoro wa ramani ya bara la Afrika . Mwanga wa jua lenyewe ni rangi ya manjano ishara ya tumaini licha ya matatizo yawakumbao waafrika.

Mchoro wa mtu chini kushoto mwa jalada la mbele. Amevalia kofia, ana fimbo mkononi na amekalia kiti cha kifahari…pia amechorwa kwa rangi nyeusi. Anaashiria kiongozi(kigogo) wa kisiasa tena mwafrika.

+Mchoro wa maji hasa huenda ni bahari kati ya mchoro wa ramani ya bara la Afrika na yule mtu mwenye kuketi kwenye kiti cha kifahari. Ni kweli kwani bara la Afrika limezungukwa na bahari.

Rangi zipo pia kwenye jalada na ni kama zifuatavyo:
-Nyeusi imetanda sana na hata kukolezwa zaidi ya rangi nyinginezo. Inatumika kuashiria yafuatayo…

a)jumuia ya Afrika.

b)mauti au kifo.

c)matatizo aina aina.

d)kiza au majira ya usiku.

-Manjano imetumija kwenye mchoro wa jua na maandishi mbele na nyuma mwa jalada. Rangi hii ina maana kuu ya…

a)mwangaza.

b)tumaini.

-Kijivu pia imetumika japo kwa mbali sana. Ina maana ya…

a)mwanga wa kiasi.

b)mwanga.

c)wema wa shaka au matatizo.

-Udhurungi inaonekana kwa mbali pia. Ina maana ya…

a)utajiri.

b)ufalme.

-Nyeupe ipo japo lazima uwe mwangalifu na inaashiria…

a)wema.

b)bahati.

Hivyo basi, jalada hili ni kama muhtasari wa Tamthilia nzima jinsi tutakavyoona kwenye uchanganuzi wake wa kine mbeleni.

Hii yatutimizia wajibu wa jalada kwa tamthilia hii na hivyo basi kuwa mwafaka na faafu ya kitabu na yaliyomo jumla.

2.8 4 votes
Article Rating
7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments

Very grateful

thank you

thankful for it

Iko Sawa my god bless

Shukrani kwa kazi nzuri

Thanks for that

Asanti sana